Kuelewa Itikadi Za Ubatizo

Maji, Damu (Moto), na Roho

Mimi, ndugu na mchungaji Rob Coones, nawasalimu katika jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Kusudi langu la kuandika nakala hili ni kuwatia changamoto na kuwatia moyo katika injili ya Kristo. Tutakuwa tukiingia katika maswala magumu ambayo haya hitaji jibu za kidini au wazo la mtu binafsi.

Twahitaji kuzingatia maadiko. Hebu tuanze kwa kuweka msingi wa kimaandiko. Waefeso 4:4-6 “Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.”

Twahitaji kwenda msitari baada ya lingine, pia hatua kwa hatua. Maandiko matakatifu yanafundisha kuhusu Mungu mmoja, twaelewa Mungu Baba (kuhusiana na ulimwengu wa Kiroho), Mungu Mwana (kuhusiana na hali ya nafsi, mpatanishi kati ya Roho wa Mungu na mwanadamu), na Roho yule ajaye kwetu, mwili wa kristo).

Kwa hivyo, twasema Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Ndio! Wote ni mmoja. Namna pia ulivyo na roho, nafsi na mwili, ila wewe ni mmoja.

Tunge’anza kuzungumzia mafundisho kuhusu utatu wa Mungu, ila tuangalie yanayo tuhusu katika mambo la ubatizo. Sababu yangu kutaja utatu wa Mungu ni kutaka watu wajue umuhimu wa kutofautisha.

Neno la Mungu linaeleza katika 1 Yohana 5:8 “Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, [Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.” Haya ya 1 Yohana 5:9, “Kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba ameshuhudia Mwanawe.” Tutakua tukitumia andiko hili kama andiko la msingi kwenye somo letu, kuhusu ubatizo. Ni vizuri kuelewa ubatizo, tutaigawa katika vipengele vitatu: - ubatizo wa Maji, ubatizo wa Damu na ubatizo wa Roho. Waebrania 6:1-3 inasema “Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na imani kwa Mungu, na wa mafundisho ya ubatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele. Na hayo tutafanya Mungu akitujalia.” Naomba msamaha kwa kusema hili �katika makanisa mengi hakika hawafundishi mafundisho ya kweli kuhusu ubatizo, ni kwa sababu hawaja elewa zaidi.

Jambo la mwisho ambalo Yesu alinena akipaa mbinguni, liko katika kitabu cha Matayo 28:19 “Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.” Tunakuta ya kwamba agizo hili lilitimizwa na kanisa la kwanza katika kitabu cha Matendo ya Mitume, kwa sababu walikwenda huku na huko, wakibatiza kwa jina la Yesu Kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi.

Kwa hiyo, tuchimbue kwa undani. Neno lasema kwamba mtu mwenye busara huona jambo kwa mbali. Lengo langu hapa sio kutaka kuwashawishi ili muingie katika dini jipya au kikundi cha watu (utatu, umoja na kadhalika). Mwito wangu ni kuhubiri na kufundisha neno la Mungu na kulitetea. Kwa hivyo, naomba tuweke wazi kotukuelewa kwa mafundisho ya ubatizo.

Ubatizo Wa Maji

Wengine husema kwamba hakuna umuhimu wa ubatizo. Kwa hivyo; tuzingatie Yesu Kristo, kama mfano wetu, akiwa Mwana wa Adamu na Mwana wa Mungu ambaye alijifanya mwenyewe pacha, yaani yeye ni Bwana na ni Kristo, katika hali hiyo aliona kuna umuhimu wa kubatizwa katika maji mengi, ili ijulikane kama sababu nzuri yaku zingatia. Amina!

Wakati mwengine twaweza elekea kwenye andiko katika 1 Wakorintho 1:17“Maana Kristo hakunituma ili nibatize, bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabadilika.” Watu wengi hutumia andiko hili kwa hali ya kujifariji kana kwamba hawahitaji kubatizwa wala kubatiza. Naomba niseme jambo hili namna nilijuavyo. Biblia inasema wazi; kama waweza rudi nyuma kidogo ukasome yale Mtume Paulo aliyonena katika 1 Wakorintho 1:12-16 Paulo hakuwa kinyume na ubatizo. Alisema kulingana na lile neno ya kwamba alibatiza na akapana majina ya wale walio batizwa.

Paulo aliendelea kusema katika kifungu cha maandiko kwamba Yesu alimtuma ahubiri Injili, na Injili ambayo alimtuma ahubiri inatuagiza kubatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Wateule, vile vile twahitajika kuzingatia kile kilichoandikwa katika Marko 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiye amini atahukumiwa.” Tena naomba tuelewe, msitari baada ya lingine. Amina!

Sasa tutizame katika Mathayo 28:16-20 “Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu. Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka. Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” Amina!

Twajua ya kuwa haya ya 16, inadhihirisha ya kwamba wanafunzi kumi na moja walikuwapo (Yuda alikua tayari amejinyonga). Haya ya 17; yatueleza ya kwamba wengine katiyao walikuwa na mashaka; ndio maana Yesu akaongea katika hali ya fumbo. Tutakwenda moja kwa moja katika kitabu cha Matendo ya Mitume (matendo ya kanisa) na tuone jinsi wanafunzi wale waliokua hapo, namna walivyotimiza yale Yesu aliyo waagiza katika haya ya 19, ambayo kanisa la dunia linaita “Agizo Kuu.” Matendo 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” Je! Petro alikosea? Twajua lah! Petro hakukosea. Mungu atusamehe tusifikirie hivyo, alikua akitimiza agizo kuu ambalo Yesu alihitaji yatendeke kulingana na Mathayo 28:19.

Wengine huamini ubatizo katika Matendo 2:38. Nazungumzia ubatizo wa kiroho pekee. Ni wazi kwamba andiko hili la zungumzia kuhusu ubatizo wa maji na roho. Waweza kuona kwamba si katika mpangilio wa kila wakati. Tutalifikiria hili punde kidogo. Mathayo 28:19 inasema, jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, sasa mmeelewa ya kuwa nimeweka msitari kwenye neno jina. Halijataja majina, bali imetaja jina. Neno Baba si jina, bali ni cheo. Neno Mwana si jina, bali ni cheo pia. Neno Roho Mtakatifu pia ni cheo. Naweza kusema kuwa baba ni wengi na pia wana ni wengi, sio cheo kiwezacho kuondoa dhambi, wala hakuna uwezo sasa, kama angetaka tubatize katika vyeo, angetumia majina haya kwa wingi yaani �majina’ bali alisema katika �jina.’

Biblia inasema hakuna jina lingine lililopewa wanadamu kwa kuokolewa kwao, na hilo ni jina la Yesu Kristo. Ndiyo maana Petro na wengine walibatiza katika jina la Yesu Kristo. Katika kitabu cha Matendo ya Mitume, hautapata Mathayo 28:19 ikitimizwa katika njia yoyote ile. Kanisa lile la kwanza lilibatiza katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo kwa ondoleo la dhambi. Wateule, jambo la muhimu ambalo mwaweza fanya ni kuona dhambi zenu zimesamehewa. Hakuna jambo muhimu kuliko hilo. Maandiko ya kuzingatia zaidi ni Matendo 2:38; Matendo 8:12-16; Matendo 10:47 na Matendo19:5.

Labda mtu aweza jiswali “kosa hili lilitokana na nini au ilikua je ili iwe hivyo?” Kanisa Katoliki la “NINICE” katika mwaka wa 321 baada ya Yesu kuzaliwa, ilibadilisha itikadi za ubatizo kuacha kutumia jina la Yesu Kristo, kinyume na namna mitume walikua wakitumia katika kitabu cha matendo, ila wakaweka vyeo (Baba, Mwana na Roho Mtakatifu).

Matendo 4:10-12 “Na ijulikane kwenu nyote, na kwa watu wote wa Isreali ya kwamba katika jina la Yesu Kristo wa Nazarethi, ambaye mlimsulibisha, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, hata kwa yeye huyu mtu amesimama hapa mbele zenu, akiwa mzima. Hili ndilo jiwe ambalo lililo kataliwa na waashi ambalo limekua jiwe la pembeni.” Hamna wokovu kwa mwigine, kwa kuwa hakuna jina lingine chini ya mbingu walilopewa watu kuokolewa kwalo. Tunaona hakuna ondoleo la dhambi katika jina lingine ila jina la Yesu pekee.

Wateule, twaomba kwa jina la Yesu, twakemea mapepo kwa jina la Yesu, twawawekea wagonjwa mikono kwa jina la Yesu. Hakuna jina lingine lililopewa wanadamu kuokolewa kwalo. Yeye ni mlango, njia, kweli na uzima. Yeye ni mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu. Usilionee haya jina la YESU.

Twaona hapa kwamba Roho Mtakatifu huja kwa jina la Yesu. Yohana 14:26“Bali mfariji ambaye ni Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka katika jina langu atawafunza mambo yote, na kuwakumbusha yote niliyo waambia.” Kwa hiyo kama tukibatiza katika jina la Roho Mtakatifu, twaona kuwa jina ni Yesu. Amina!

Hapa Yesu amekuja kwa jina la Baba yake. Yohana 5:43 “Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.” Kama tunabatiza katika jina la Baba, hilo jina ni Yesu. Sasa sini rahisi? Ni mtego wa ibilisi kuwaingiza katika shimo la maji ya vyeo: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Kama ulibatizwa katika jina la vyeo, ningependa kumtafuta mtumishi wa Mungu ambaye anaamini katika jina la Yesu na nguvu za jina la Yesu Kristo, na aliyebatizwa katika jina la ajabu la Yesu Kristo kwa ondoleo la dhambi. Waweza kusema, “ndiyo sidhani ni muhimu;” jibu langu ni “una uhakika? Waweza kuwa unanungunika moyoni mwako. Tena, kumbuka kwamba ilimchukua Yesu mda akimtafuta Yohana. Walibatizwa tena katika jina la Yesu. Matendo 19:4-5 “Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakaye kuja nyuma yake, yaani, Yesu. Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.”

Twaweza vile vile soma kuhusu wale waliobatizwa katika Roho Mtakatifu, namna walivyoendelea kukamilisha ubatizo huo katika jina la Yesu. Matendo 10:46-48 Kwa kuwa waliwasikia wakinena katika ndimi, wakimtukuza Mungu. Halafu Petro akajibu �mtu aweza kuzui maji ili hawa watu wasibatizwe, ambao wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi? Kwa hivyo akaamuru wabatizwe katika jina la Bwana. Halafu wakamsihi akae huko siku kadhaa.

Ndugu na dada zangu, andiko hili latusaida kuelewa umuhimu wa ubatizo katika jina la Yesu. Twaona kuwa, wale walijazwa na Roho Mtakatifu waliagizwa kubatizwa katika maji, katika jina kuu la Yesu Kristo. Nimeona ni vigumu kuamini kwamba mtu hawezi kuona umuhimu wa kubatizwa katika jina la Yesu. Tafadhali, katika hali ya maombi, zingatia hili, kama ulibatizwa katika majina ya vyeo, ubatizwe tena. Nilikua katika mafundisho fulani, na kwa neema ya Mungu, akaniongoza mpaka ufahamu huu. Nilikua nikihubiri Injili, nikiona Mungu amefanya miujiza, uponyaji na kualika watu ili wamjie Kristo wapate kuuona ufalme wa Mungu. Hata hivyo nilikuta kwamba ni muhimu kubatizwa tena kwa ondoleo la dhambi.

Nadhani kwamba ningekua nimeenda kuzima kabla niufikie ufunuo huu. Naweza kujibu kwa kusema kwamba dhambi haliwezi kutambuliwa bila kulielewa. Lakini, nitasema ningekataa ubatizo wa maji mengi katika jina la Yesu Kristo sasa, ningekuwa katika hatari ya moto. Hili si chaguo la kidini, bali ni fundisho la kidini, hili ni neno la Mungu.

Omba ili Mungu akufanye vile alivyo mfanya Mtume Paulo katika barabara iliyonyoka na kufungua ufahamu wako. Ndugu, Paulo alienda huko Dameski na akabatizwa katika jina la Yesu, na magamba yakatoweka machoni mwake. Ndiyo, Paulo alikua amejitoa sana kwa Mungu. Alifikiria alikuwa mzuri. Lakini alikua katika makosa. Je! Una unyenyekevu wa kutosha kwa kuzingatia neno la Mungu? Hebu, tuendelee katika maswala haya ya ubatizo. Ningependa kusema kwamba mtu anapofariki huzikwa. Maandiko husema kwamba tumesulibishwa pamoja na Kristo. Tumezikwa pamoja na Kristo katika ubatizo. Mtu anapofariki, hanyunyiziwi vumbi juu yake. Anazikwa ndani ya udongo. Nisemacho ni kwamba, mbatizapo mtu katika maji, hamnyunyizii maji juu yake, bali mnamzamisha ndani ya maji mengi.

Tafadhali, tufanye uchunguzi juu ya somo lisilo eleweka, yaani ubatizo wa wafu katika 1 Wakorintho 15:29-31 “Au je! Wenye kubatizwa kwa injili ya wafu watafanyaje? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao? Na sisi, kwa nini tumo hatarini kila saa? Naam, ndugu, kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu, ninakufa kila siku.”

Twajua dini fulani watu husimama kwa niaba ya waliokufa na wanabatizwa ubatizo wa wafu, na wanatumia andiko hili kwa kulinganisha na kudhibitisha mafundisho yao, ambayo ni mafundisho yasio sawa. Kama ukitambua kifungu cha 31, Paulo anasema �nakufa kila siku’ ndiyo, alibatizwa.

Tunapoingia katika ufahamu wa kwamba tumesulubiwa pamoja na Kristo, halafu tumekufa. Paulo aliandika vile vile katika Wagalatia 2:20 “Nimesulubiwa na Kristo, lakini ni hai, wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani mwangu, na uhai nilionao sasa katika mwili, ninao katika imani ya mwana wa Mungu, ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.” Tufikapo katika kufahamu kwamba tumesulubiwa pamoja na Kristo, tumekufa na tunahitaji kuzikwa. Hii ndiyo sababu hatubatizi wafu.

Kama mtu haelewi kwamba hakuna haja ya kuwabatiza, utapata watu humwagiwa maji kama ubatizo. Hii ndiyo maana hatubatizi watoto. Kwa sababu hawana ufahamu wa kutosha ili kuelewa ubatizo, na kufisha matendo ya mwili na ubinafsi wa kila siku. Mpaka tungojee watoto wafikie umri au kiwango wa kuamua wenyewe kwa Yesu Kristo, na wanapojua kuamua kuacha mambo ya dunia hii.

Mtu anaweza kuuliza, ni umri gani unaofaa? Wengine wanasema ni umri wa kuajibika. Tafuteni mtumishi wa Mungu ambaye anaongozwa na Roho Mtakatifu akushahuri na akusaidie kufanya uamuzi wa kiungu. Ninaweza kusema, nimewazuia wengine wenye umri wa miaka 20, 30, 40 na kadhalika, kwa sababu hajafariki kiroho, yaani hawaja mpokea Bwana Yesu kama Mwokozi wa maisha yao, kikamilifu. Ila upande mwengine nimeshabatiza watoto wa umri wa miaka 12.

Natumai, mawazo haya yanaweza kukusaidia kuelewa kwamba kama ulibatizwa ukiwa mtoto, au katika vyeo - Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, lakini zingatia kubatizwa katika jina la Bwana na Mwokozi Yesu Kristo.

Ubatizo Wa Damu (Moto)

Tunaanza kwa kueleza kuhusu damu na moto. Tunaingia kwenye maandiko katika kitabu cha Yoeli 2:31 “Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishiyo.” Wakati andiko lasema mwezi utageuka kuwa kama damu, twaelewa hii kuwa ni moto. Maranyingi katika maandiko waona kwamba damu na moto vyabadilika.

Sasa, kama tukirudi nyuma katika maandiko, tutajua kwamba Yesu alibatizwa kwa damu msalabani hapo Kalvari. Twajua kwamba ubatizo unamaanisha kuzikwa (mazishi), kuzamishwa ndani ya maji mengi. Yesu alifunikwa kabisa na damu kwenye fuvu. Mgongo wake ulikua umelimwa kama shamba, misumari miguuni na mikononi mwake, na kudungwa ubavuni mwake. Tena, alifunikwa kabisa na damu.

Sisi ni warithi pamoja na Kristo kupitia kumwaga damu yake na kubatizwa katika damu yake pale Kalvari. Warumi 6:3-5 “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;” Neno lasema kwamba tulisulibishwa pamoja naye pale Kalvari na tumefufuka pamoja naye. Bwana asifiwe!

Hapo ndipo twapata uzima wa milele tele. Yesu ni mlango, njia na uzima. Hakuna njia nyingine kwa kwenda uzimani, ila kwa yeye. Twajua neno latufundisha kwamba dhambi ilikuja ulimwenguni kupitia mtu mmoja na iliondolewa kwa kupitia mtu mmoja. Warumi 5:17 “Kwa kosa la mtu mmoja dhambi iliitawala kwa mmoja, ni zaidi kwa wale wapokeao wingi wa neema na kipawa cha haki watatawala katika uzima kwa mtu mmoja - Yesu Kristo.”1 Wakorintho 15:20-22 “Lakini sasa Kristo amefufuka kutoka wafu, na akawa limbuko la wale waliolala kwa kuwa kupitia mtu mmoja mauti ilikuja na kwa mtu mmoja ufufuo wa wafu. Kwa Adamu wote hufa, vivyo hivyo kwa kupitia kwa Kristo wote wataishi.” Kwa hivyo tunaelewa kwamba dhambi iliingia ulimwenguni kwa sababu ya kuanguka kwa mwanadamu pale bustani mwa Edeni, ikatufanya tuwe warithi wa mauti. Yesu akaiharibu na kutufanya warithi wa uzima.

Damu ya Yesu haikumwagika kwa dhambi ya kukusudia (kutaka). Watu wengi hudhani kwamba wanaweza kuishi maisha ya dhambi wakifikiri ya kwamba damu ya Yesu iko kwa ajili ya dhambi za kukusudia. Hili ni kosa kubwa. Neno latufundisha katika Waebrania 6:4-6 “Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanya washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedheni kwa dhahiri.” Andiko lingine ni katika Waebrania 10:26-27 “Maana, kama tukifanya dhambi la kusudi baada ya kupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.”

Damu ya Yesu iliosha dhambi zote zilizokuja duniani kupitia kwa kuanguka kwa mwanadamu katika bustani. Kwa kuwa wote wametenda dhambi nakupungukiwa na utukufu wa Mungu. Wengi wanafanya makosa kwa kudhani kwamba wataendelea kwaku kusudia na kualika damu ya Yesu. Tena hili ni kosa kubwa sana. Ndugu na dada zangu, tumeingia katika agano jipya; kumbuka mmoja kwa maji, mmoja kwa damu na wingine kwa Roho Mtakatifu. Hebu! tutazame mambo na mifano kadhaa yatakayo tusaidia kuelewa kabla hatujaendelea katika somo kuhusu dhambi za kukusudia.

Tunaporudi kutazama katika agano la maji, lilivunjwa walipokula lile tunda wa ule mti uliokatazwa katika bustani la Edeni. Ni hapo ambapo twaona agano lingine likifanywa. Agano la damu lilianzishwa wakati damu ya wanyama ilimwagwa ili kufunika Adamu na Hawa kwa nguo za ngozi baada ya kumkosea Mungu. Hili latusaidia kuelewa kwa nini Mungu hakukubali sadaka za Kaini, ya mazao ya ardhi (mfano wa uzima wa maji).

Ikiwa ni mazao ya kwanza (malimbuko) ya Kaini, ungedhani ingependeza Mungu, lakini haikuwa namna hiyo. Mtu anaweza kujiuliza “kwa nini?” Jibu ni kwamba, kwa sababu agano la maji lilivunjwa. Abeli alitoa sadaka ya damu, ndiyo iliyohitajika, na Mungu akakubali. Tuliona kwamba agano la maji lilivunjwa katika bustani. Mwisho wa agano la maji lilionyeshwa kwa gharika wakati wa Nuhu.

Sasa, twaelewa kwamba agano hili lilikua agano la damu. Damu ilikuwa ikinyunyizwa wakati wote wa agano la kale. Twajua wanyama walitolewa kafara ili kurudisha dhambi nyuma. Twagundua kwamba kafara ya damu iliisha wakati Yesu Kristo alifanyika kafara akakubalika. Yesu alisulibiwa hapo Kalvari, kwa hivyo, twajua kuna agano jipya ambalo tumeingia sasa nao niwa Roho. Ndiyo maana twaomba kwa Roho, twatembea katika Roho na twamwabudu Mungu katika Roho. Roho yetu wanadamu umeshikana mbali na Kristo, iko mbali naye. Kwa hivyo, nimeeleza haya ili yatusaidie kuelewa lile lililosemwa katika Waebrania 10:26-27. Tunatumia maelezo yaha ili kuelewa ni kwa nini damu ya Yesu Kristo haifuniki dhambi za kukusudia.

Tumeshaingia katika agano jipya. Kama vile tu sadaka ya Kaini ilivyo kataliwa na Mungu kwa sababu tayari kulikua na agano jipya ambalo limeanzishwa. Kwa hivyo mtu aweza kudhani kuwa nimesema damu ya Yesu ilikataliwa. Sivyo, nisemavyo! Nimesema ya kwamba damu ya Yesu ilikubaliwa na hiyo ndiyo iliyotuleta katika uzima wa milele katika Kristo.

Tunajazwa na nguvu za Roho Mtakatifu na hatuwezi kutenda dhambi kulingana na 1 Yohana 3:9 “Kila aliye zaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.” Hii ndiyo sababu hatuendelei kutoa damu kama kafara. Amina! Tafadhali, msifikiri natakakupinga damu ya Yesu. Lah, hasha! Hauwezi kuingia katika agano la Roho, mpaka upitie katika damu ya Yesu. Itachukua mda kwa kuingia undani kabisa. Naendelea kurahisisha mambo na kuzingatia misingi ya ubatizo. Mimi, kama hivyo Paulo, alisema eti �nazungumza nanyi kama watu wa Kiroho’ lakini aliendelea kueleza kwamba aliwaona wakiwa watu wa kimwili - au wenye mawazo ya kawaida. Hii ni kweli maana neno la Mungu limefichwa kwa watu wengi, kwa sababu ya upofu wa mawazo ya kimwili.

Tutaendelea kujifunza na kutambua mawazo ya kimwili au vyombo vya udongo. Hebu! Tuangalie katika lengo tofauti au nguvu tofauti. Tukitazama dunia, twaona ilibatizwa katika maji ya gharika ya wakati wa Nuhu. Halafu, 2 Petro 3:7 “Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasio mcha Mungu.” Utakaso mwingine utakua kwa moto wakati dunia itateketea kabisa. 2 Petro 3:10 “Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufunuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.”

Dunia itapita katika batizo zote tatu. Dunia imeshabatizwa katika maji tayari, na twasoma kwamba itabatizwa katika moto pia. Twajua kwamba itapitia katika mabadiliko, ikibadilika kutoka uovo kwenda utakatifu, ambao ni ubatizo wa Roho kuelekea dunia, au kubadilishwa kwa dunia kama unajifunza kutizama. Mungu kawaida hufanya kazi kwa mitindo. Warumi 1:20 “Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru” Twawezakuwa na mitindo yasiyo onekana (Roho) namna ulimwengu unavyo uona. Halafu, tunajua dunia hii, au ningesema vyombo vya udongo (mwili) vitafanya jambo kama hayo. Tunatimiza ubatizo wa maji, damu na wa Roho Mtakatifu. Kuna ubatizo wa moto kwa wateule wa Mungu, (wana wa Mungu), na halafu kuna ubatizo wa moto kwa wana wa ulimwengu. Ubatizo wa moto kwa wateule wa Mungu na ubatizo wa moto kwa waovu, au wana wa ulimwengu. Ni ubatizo tofauti. Ubatizo wa moto kwa wana wa Ibilisi, itakua kutupwa katika lile ziwa la moto wa milele. Watateketea kabisa katika miale ya moto ya Jehanamu. Hii inaambatana na maaandiko katika Waebrania 10, inayo ongea kuhusu moto wa wivu wa Mungu. Kwa wateule, si kutupwa katika ziwa la moto, bali ni kubatizwa katika moto wa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu kwetu, kama wateule, ni moto ambao uosha na kututakasa. Ni vizuri tukumbuke kwamba Roho Mtakatifu aliishi ndani ya Yesu, ambaye ni Roho wa Baba; kumbuka ni Roho wa Baba ambaye atuonyaye, na ni Roho huyo huyo atufarijiye.

Wajua kuwa nazungumza kuhusu jukumu la Baba. Jukumu la Baba ni kufunza, kuelekeza, kulinda, kuadhibu na kurekebisha. Shukuru Mungu tunaye Baba wa mbinguni, tutembeapo katika njia zisizo mpendeza, Mungu Baba atuadhibu kupitia moto wa Roho Mtakatifu. Waebrania 12:5-9 “Tena mmeyasahau yale maono, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, wala usizimie moyo ukikemewa naye; maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, naye humpiga kila mwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wawili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?” Kwa kuwa yeye Bwana ampenda mwana, ndio sababu anamwadhibu. Inaendelea kusema kama hawezi kutuadhibu sisi ni wana wa haramu, au ningesema kwamba hatuna Baba wa mbinguni. Hii ndiyo maana, ndugu zangu, twahitaji kutimiza neno la Mungu. Alituma Roho wake kwetu ili tuweze kupokea nguvu kuwa wana wa Mungu. Alitupa nguvu za kutoka na kutengwa na ulimwengu. Hii ndiyo maana twahitaji kupokea ujazo wa Roho Mtakatifu. Sasa, twende katika sehemu nyingine ya mafundisho yetu - ubatizo wa Roho.

Ubatizo Wa Roho

Yohana mbatizaji alisema, kuna ajaye baada yake ambaye hana uwezo wa kufungua gidamu za viatu vyake. Aliendelea kusema kwamba Yesu alibatiza katika Roho na moto. Naomba muweze kuyaelewa vizuri namna Roho anavyosema kuhusu jambo hili. Baadhi ya wandugu na marafiki wa kipentekoste wana maoni yao kuhusu ubatizo wa Roho. Nimechangia pamoja nao katika ufahamu, bali nitajaribu kuchimba kwa undani kidogo katika somo hili na kuwapa changamoto.

Yesu alisema ni lazima arudi kwa Babaye ili amtume msaidizi mwingine, Roho Mtakatifu, mfariji. Ahadi aliyoifanya Yesu imetimia. Hebu! tusome Matendo 2:1-4 “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukajaza nyumba yote waliokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizo gawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila umoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyo wajalia kutamka.” Hebu, tuchambue vizuri jambo hili, kwa sababu watu wengi hutumia maandiko haya kama msingi wao wa mafundisho ya uongo. Kuna mafundisho ya uongo, na mapepo huingia na kutafsiri Neno vibaya. Biblia inatufundisha kwamba Neno si tafsiri la mtu binafsi.

Ubatizo wa Roho Mtakatifu si kwa sababu ya kunena katika ndimi tu, unabii au kukemea mapepo. Waovu au wana wa ulimwengu wanaweza kufanya hivyo na hawajajazwa na Roho Mtakatikfu. Sasa, mngenisamehe! Sijakataa vipawa au karama za Roho Mtakatifu. Biblia inasema mwerevu huona mwisho wa jambo mapema. Matayo 7:22-23 “Wengi wataniambia siku ile; Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni ninyi watendao maovu.” Ni lazima tuishi matendo kuliko kutaka zaidi kunena kwa lugha, kutabiri au kushughulikia vipawa vya Roho Mtakatifu. Maandiko yanatufundisha kwamba vipawa na mwito si vya toba. Nataka kueleza kuhusu vipawa vya Roho Mtakatifu na vipawa vya Roho. Vipawa vya Roho Mtakatifu huja kufuatana na toba kwa hayo ni uzima wa milele. Vipawa vya Roho huja bila toba na vina angukia mwenye haki na asiye na haki. Nadhani kwamba kama unataka ushahidi wa vipawa vya Roho Mtakatifu, jambo la kutizama ni mtu anayetembea sawa sawa na neno la Mungu.

Yesu aliwaambia wanafunzi waende na wangojee mpaka watakapopokea nguvu. Mwaweza kuuliza, nguvu za kufanya nini au nguvu gani? Ilikua nguvu za kunena kwa lugha? Lah! Ni nguvu za kutoka katika dunia na kuwa wateule. Nguvu si za kuishinda ulimwengu tu, bali na miungu ya ulimwengu. Nguvu za kushuhudia, Amina! Ndiyo, tuliona katika Biblia kwamba walipojazwa na Roho Mtakatifu, walinena kwa lugha kama alivyowawezesha. Ninaweza kuendelea kusema kwamba watu wengi wanapokea vipawa vya Roho Mtakatifu siku hizi na saa hii hunena kwa lugha. Na hii sio dhibitisho la mwanzo wakujazwa na Roho Mtakatifu. Pia Biblia inasema, walionekana kama wamelewa mvinyo katika masaa ya asubuhi, pia kulikuwa na ndimi za moto juu ya vichwa vyao. Pia inanena kuhusu upepo mkali uliokua ukivuma. Je, ni lipi kati ya hayo utatumia kama dhibitisho? Yesu akasema, nendeni mkangojee mpaka mjazwe na nguvu. Hakusema mpaka mkanene kwa lugha.

Nataka kusema kwamba nimewaona watu wasio jazwa na Roho wakinena kwa lugha na wakifanya kazi ya vipawa kama uponyaji, miujiza na neno la ufahamu, na kadhalika. Lazima tuwe makini tunapofundisha kwamba ishara ya kwanza ya kujanzwa kiroho ni kunena kwa lugha. Ningependa kuwapa moyo kutafuta vipawa vya Roho Mtakatifu; neno la hekima, neno la maarifa, imani, karama ya uponyaji, miujiza, unabii, upambanuzi wa roho, lugha, tafsiri za lugha. Vipawa hivi ni kwa ajili yetu, sisi Wakristo ili kutusaidia kutembea katika Roho, kutusaidia kukua katika neema na ufahamu wa Bwana na kutusaidia katika ufahamu wa Bwana na kutusaidia katika vita dhidi ya mkuu wa giza (shetani). Tunahitaji vipawa vyote vya Roho.

Shabaa yangu nikutaka mjue hatari iliyo katika kufundisha, kwamba dhibitisho la mwanzo la kujazwa kwa Roho ni kunena kwa lugha. Sineni kinyume na vipawa vya Roho Mtakatifu. Biblia inasema katika 1 Wakoritho 14:5 “Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kuhutubu, maana yeye ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, ispokua afasiri, ili kanisa lipate kujengwa.” Unabii na wakutamanika au wamuhimu kuliko kunena kwa lugha. Kama kunena kwa lugha ni Roho Mtakatifu, hiyo ni kusema kwamba lugha ni muhimu kuliko Roho Mtakatifu; na twajua vizuri kuliko hayo. Hakuna kitu kilicho muhimu kuliko Roho Mtakatifu. Je, inawezekanaje kuwa na kitu cha muhimu kuliko Roho Mtakatifu? Kwa hiyo hatuwezi hatuwezi kusema eti kunena kwa ndimi ni kipawa cha Roho Mtakatifu. Ni lazima tuelewe kwmaba vipawa si dhibitisho ya maisha yaliyojazwa na Roho. Tunajiachilia wazi kwa uongo huo wa mapepo tunapoamini hivyo. Biblia yasema kwamba mvua hunyesha kwa wenye haki na wasio na haki, na kuhusu ngano magugu. Imeandikwa katika Yoeli 2 :28 “Hata itakua, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wataona maono.” Andiko halijasema eti kwa watoto wake au wateule pekee, inasema wote.

Ningeweza kuendelea kusema kama vile Paulo alivyosema, “ninanena katika lugha kuliko ninyi nyote, lakini siwezi kufundisha, hiyo ndiyo dhibitisho ya Roho Mtakatifu. Miaka mingi, nimeshuhudia watu wengi ambao wamepokea Roho wa Mungu, lakini hawakupokea karama ya kunena kwa lugha. Waliadhiriwa na mafundisho kuhusu lugha kama dhibitisho la Roho Mtakatifu, wengine hata walipotoshwa katika imani yao kwamba hawana Roho wa Mungu. Wacha tufundishe watu kutafuta na kutamani vipawa vya Roho Mtakatifu na vipawa vya Roho. Biblia husema katika 1 Wakorintho 14:22 “Basi, hizi lugha ni ishara, si kwao waaminio, bali kwao wasionamini lakini kuhutubu si kwa ajili yao wasioamini, bali kwa ajili yao waaminio.” Haijasema ilikua kwa wanaoamini au wakristo. Ndiyo maana Biblia inasema anashangazwa na wanaohitaji ishara. Kwa hivyo, ningependa kuuliza ni kwa nini kanisa duniani au wakristo wanasema kwamba ishara au dhibitisho la Roho Mtakatifu.

Nimeshuhudia wanaume na wanawake wanaoishi maisha ya dhambi na wanatamani mambo ya kimwili naya duniani, ila wako katika maisha ya kunena kwa lugha, kama dhibitisho la Roho Mtakatifu. Wanapokuja kanisani ni kama mvua, wananena kwa lugha na kuanza kutabiri. Kwa sababu ya mafundisho ya kwamba lugha ni dhibitisho ya kuwa na Roho Mtakatifu, nawasihi muweze kuchunguza unafikiri, eti Mungu amewajaza Roho wake nabado wanazidi kuishi maisha ya dhambi za kusudi. Ndio maana nasema mafundisho hayo ni hatari kwa sababu yanaelekeza watu kuamini kuhukumiwa.

Pia twajitaji kuwa makini tunapofundisha watu kwamba wanapata wokovu bila vipawa vya Roho Mtakatifu. Biblia inasema katika Warumi 8:9 “Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokua na Roho wa Kristo huyo si wake.” Bila Roho wake ninyi si wake. Awezaje kusema ninyi si wake kama mkizaliwa mara ya pili? Lazima muwe na Roho wa Mungu ili muokoke. Mara nyingi makanisa mengi ya ulimwengu hutenganisha vipawa kutoka kwa wokovu. Twajua kwamba tunapookoka tunapokea Roho wa Yesu Kristo. Amina! Huyo ndiyo Roho Mtakatifu.

Ndugu na dada zangu, vipawa vya Mungu ni sisi kuvijaribu. Omba Mungu awape vipawa vya hekima na upambanuzi ili muweze kujaribu kila roho kulingana na namna mmejifunza katika somo hili na muelewe kwamba ni ya Mungu. Watumishi wengi wa Mungu wamekuwa wakibadilisha msimamo wao wa kimaandiko jinsi walivyokuwa katika neema na ufahamu wa Mungu. Ila tu uwe mmoja wa wale Biblia inataja katika 1 Wakorintho 8:1-3 “Na kwa habari ya vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sisi sote tuna ujuzi. Ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga. Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lolote bado, kama impasavyo kujua. Lakini mtu akimpenda Mungu, huyo amejulikana naye.” Ninatumia na kuomba sana usiwe yule ambaye Biblia inataja kuwa anajua kitu na hajui chochote jinsi ipasavyo kujua. Amina!

Ninajaribu kuwasaidia kurekebisha mafundisho yenu, ombeni sana Mungu awaondolee majivuno ili muweze kujichunguza ninyi wenyewe jinsi mnavyohamuru kutenda na kuona kama mko katika imani. Kusudi langu ni kuwapa changamoto katika maandiko na katika mafundisho. Biblia inasema kama mtu akifundisha mafundisho tofauti kinyume na yale Yesu aliyohubiri, na ahukumiwe. Najua mwahitaji kuwa na mafundisho ya kweli.

Katika hali ya maombi, zingatia, ongea na Bwana, na atakuongoza katika kweli yote. Tena, sijaribu kuwaingiza katika kweli yangu binafsi. Tena, sijaribu kuwaingiza katika dini jipya. Hii sio mafundisho ya umoja au utatu. Haya ni mafundisho ya Yesu Kristo. Siendi kinyume cha utatu au umoja, ila yote yana ukweli wa kibiblia na kasoro za mafundisho yao. Sikuitwa kutetea hata moja ya hayo. Nimeitwa kutetea Neno la Mungu.

Somo hili fupi laweza kuleta mabadiliko makubwa katika maisha yenu. Itasaidia kuondoa upofu wa kidini na itakusaidia kuona wakati kitu kizuri kinakuja. Mfuateni Bwana, hawezi kuwaacha au kuwasahau.

Nawashukuru kwa kuchukua mda wenu kusoma nakala hili. Nimejaribu kufanya kuwa fupi na rahisi kuhusu jambo hili. Hatukukwaruza sehemu ya somo hili. Ombeni ili Mungu awasaidie na awafungue ufahamu wenu. Kuwa pia makini kwa yale utakayoamua kufanya, kwa kuwa kama utaamua kukataa, utakua umekataa Neno la Mwenyezi Mungu aliye juu. Waweza kuwa kama Mtume Paulo, alidhani alifanya vizuri kutesa kanisa.

Miaka mingi, nimeona kazi nyingi zilizokuwa kama za Mungu zikikoma, wanapokataa mafundisho kuhusu ubatizo. Tuhakikishe kwamba tumetimize hizi ubatizo tatu. Moja inahusiana na mwili, na moja nikwa nafsi na nyingine ni kwa roho. Au tungesema Maji, Damu na Roho. Tafadhali, ninawaomba kuzingatia mafundisho haya. Kama unasoma nakala hii na hauna kanisa kwa kuabudia, nakusihi utafute kanisa zuri ambayo inafundisha neno la Mungu na kuhubiri Biblia yote katika kweli. Mungu naye atakuongoza katika kweli yote.

Tujulisheni, (tuandikinie) nasi tutapenda kusikia maoni yenu. Na ukiwa na swali, twaomba utuulize. Tutafurahi, tuko tayari kukujibu, kukuandikia kwa neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Ndugu na Mchungaji,

Pastor Rob Coones

Ujumbe huu na mafundisho mengine katika kanda ya Ndugu Mchungaji Rob Coones, yanapatikana katika mtandao, na umechapishwa na kugawanywa bila malipo. Kwa nakala au lugha nyingine zaidi, Andika kwa lugha ya Kingereza kwa anwani iliyo hapo chini, na eleza kiasa unayo hitaji kwa matumizi ya kazi ya Mungu.

Christian Temple Ministerial Association
3844 Mount Gilead Church Road
Sophia, NC 27350-8820 USA