Ninajuaje Ya Kuwa Nimezaliwa Mara Ya Pili?

...Mtu asipo zaliwa mara ya pili hawezi kuuona Ufalme wa Mungu. Yohana 3:3

Swali hili husikika kuwa rahisi kujibika, kweli ni rahisi usipo lichunguza kwa undani, lakini ulichunguzapo kwa makini, lakanganya katika hali ya kawaida mtoto anapo muuliza mama anayebeba mtoto mchanga ya kwamba �Je! Ndugu yangu mdogo ametoka wapi?� Nijibu rahisi ambalo mamaye atamjibu kwamba alitoka kwa Mungu. Au aweza kumweleza kwa undani kidogo kwamba baba yako na mimi, tumekua na uhusiano wa ndoa. Mbegu zikatoka kwa viuno vya babako na nikawa mjamzito. Mara ingine, kuna wapenzi wapitiao katika uhusiano wa ndoa na mimba haitokei. Yawezekana kizazi hakiwezi kushika mimba kwa kuwa ni tasa, hakina nguvu za uzima ndani ya mbegu. Kwa hivyo, tukiangalia hali ya maumbile, tunaelewa hali ya kiroho. Singependa kufanya mambo rahisi, ambapo kuna ongezeko la maelfu ya watu ambao wanaamini kwamba ni Wakristo na hawamjui Mungu. Au twaweza kusema, hawamjui Mungu; kwa kuwa, andiko lasema �ninatabiri kwa jina lako, kufukuza mapepo� jibu la Mungu lilikuwa �Sikujui�.

Ninajua Biblia yasema kwamba Mungu anajua vitu vyote, ila kujua anaozungumzia ni uhusiano wa kipekee na Kristo, ambao huja kwaku olewa naye. Neno hilo, kujua, hutumika wakati lisemwapo baada ya Yesu alipo zaliwa. Huu ndio uhusiano wa ndoa uzungumziwao. Kuna wahubiri kadhaa ambao uhubiri Neno, lakini mbegu zao zimekufa kutokana na kutoamini, mafundisho ya uongo, au maovu katika maisha yao. Halafu kuna wengine ambao hukaa chini ya watu wa kweli wa Mungu, na hawawezi kuona tunda la Roho katika maisha yao, na hiyo ya fanana na tumbo lisilozaa. Kumbuka, Yesu alisema, �lazima uzaliwe mara ya pili ili uhurithi ufalme wa Mungu�.

Andikolingine la kuizingatia, wale watakao vumilia hadi mwisho, wataokoka. Kwa hivyo ningeweza kusema, haijalishi ni tunda la aina gani ambalo waweza kuliona leo, kwani hatuambiwi mwisho wake kama tungeweza kufikiri, hata kwa mda mfupi tu; na fikiria wale wote tumewashuhudia kwa mda wa miaka mingi, walionekana wana wokovu na pia wana moto wa Mungu. Halafu, wanarudia dunia. Neno lasema wanaporudia dunia ina dhihirisha kwamba wao sio wa upande wetu maana yake hawaja zaliwa mara ya pili. Wengine waweza sema, ah! Hapana, wamerudi tu nyuma. Ila Yesu alisema ya kwamba hakumpoteza hata mmoja wao. Kuna mambo mengi ya kuzingatia. Nimesha shuhudia watu wengi wanaoishi kama ibilisi (Shetani) mwenyewe, na watasimama, uso kwa uso nao wakidai ya kuwa wamezaliwa mara ya pili. Hiyo siyo imani!

Yakobo alisema �nitakuonyesha imani yangu kwa matendo� . Umezaliwa mara ya pili kwa imani. Twajua ya kwamba bila imani hauwezi kumjua Mungu wala kumwona. Kwa hivyo, ukiwa na imani, utakuwa na matendo ya wokovu. Ninajua kwamba twaokolewa kwa imani kupitia neema, lakini si kwa matendo. Na hiyo haimaanishi hakuna matendo. Imani yazaa matendo. Waweza kuwa na matendo bila imani, bali hauwezi kuwa na imani bila matendo. Baadhi ya dini siku hii na saa hii, wanapeana wokovu bila kubadili mitindo ya maisha, hilo ni kosa kubwa. Tunapo fikiri neno �wokovu� ume okolewa kutoka kwa kitu fulani. Biblia yatufundisha ya kwamba ni lazima tutoke katika dunia (tutengane na dunia). Twaokolewa kutokana na mambo ya dunia, si ndani ya dunia. Tunapojazwa na Roho Mtakatifu, tunapokea nguvu. Waweza sema �Nguvu za nini?� Nguvu za kutoka katika mambo ya dunia na kwa watu waliotengwa. Ni lazima tuache kubadili Biblia ili ifae mitindo ya maisha yetu, na tubadili maisha yetu yafae Biblia.

Tunaposoma Biblia, twakuta kuwa Yesu aliandaa mitume. Neno hili �nidhamu� latokana na neno �mwanafunzi�. Wokovu ni uzima wa mwanajeshi. Ni vita inayoendelea, kupigana na mamlaka na nguvu za giza. Shetani yeye ni kama simba angurumaye akitafuta mtu ammeze. Neno la Mungu latufunza kuvaa silaha zote za Mungu. Wakristo wakuu wengi wako katika hali ya uvugu-vugu, hawakuvaa silaha, na hawaelewi vita vya kiroho. Mara nyingine wao si tishio kwa ufalme wa Shetani, kwa hivyo hawako vitani.

Unapo shika moto wa Mungu, unakuwa tishio katika ufalme wa Shetani naye atageuka kinyume nawe.

Wengine hawajatambua hiyo. Wengine hudhani kwa sababu wao ni washirika wa kanisa, au wamesema ombi fulani; kwa hiyo wameokoka. Lakini acha niwakumbushe, ni yule avumiliaye hadi mwisho ndiye atakaye okoka. Ikiwa tutavumilia hadi mwisho, huko ndiko kuokoka. Twapigana na adui na mishale ya ibilisi. Biblia yatufundisha ya kwamba kuna utungu katika kuzaa mtoto. Tunapo zungumzia kuzaliwa mara ya pili, yamaanisha kuna utungu katika kuzaa tunda la Kristo katika maisha yetu. Jinsi mama ajifunguapo mtoto, au hauwezi kuwa na urithi wowote. Paulo alinena, �Ninajitahidi mpaka Kristo afanyike ndani yenu�. Biblia pia yatufundisha kuchechemea katika mwendo wetu hadi kwenye ufalme wa Mungu. Pia yasema ujichunguze mwenyewe uone kama waweza kuwa katika imani.

Dini siku hizi na wasaa huu zinatoa wokovu usio na jitihada, hakuna kafara. Biblia yasema �ufe ili yeye aishi�. Kwa hiyo mara nyingi, watu wanataka kuwa na uzima wao na uzima wa milele pia. Lakini ni lazima upoteze uzima wako ili kupokea uzima wake Yesu kristo.

Tena, Neno la Mungu latufundisha kwamba ukijaribu kuokoa nafsi au maisha yako utayapoteza. Twataka kupata njia kutoka kwa ufahamu wako mwenyewe. Si maoni yako mwenyewe au jinsi unavyo fikiria ndivyo ilivyo. Ni jinsi neno lisemavyo ndivyo ilivyo. Ebu! tuingie katika Neno la Mungu, Neno lake ni roho na kweli, na ukweli wa hilo Neno utakuweka huru. Je! Uko katika swali kuhusu wokovu wako? Je! Wajuaje kuzaliwa mara ya pili kwako? Ebu! tuangalie katika Biblia kwa mfano wetu. Yesu aliwapata wafuasi na akawaongoza. Paulo alisema �nifuateni jinsi mimi ninavyo mfuata Kristo�.

Ningeweza kusema tafuta kanisa nzuri ambalo hufundisha mafundisho ya kweli na mtumishi wa Mungu ambaye atembeaye katika Roho. Kweli si rahisi kuzipata, lakini omba naye Mungu atakuongoza. Hawezi kukuacha udanganywe. Ukiwa mwaminifu, atakuongoza katika kweli yote. Twahitaji kuwa na ushirika hadi mwisho. Biblia yasema, �mwajua tumevuka kutoka mauti hadi uzima kwa sababu twawapenda ndugu zetu�. Pia yatufunza tusisahau kukusanyika pamoja, kwa hayo twajua kwamba imani huja kwa kusikia Neno la Mungu. Twahitaji kanisa na umoja wa wandugu. Fikiri juu ya mwanajeshi katika jeshi huko katika nchi ya ugenini akiwa mwenyewe: Hawezi kuwa na nguvu, lakini akiwa katika kundi kuna nguvu. Mmoja aweza kufanya maelfu kutoroka, na wawili waweza kufukuza elfu kumi. Kwa hivyo, tufikiriapo kuhusu dunia hii, ni ya Shetani. Yeye ni mfalme na nguvu za hewani. Yafaa kujua kwamba twahitajika kuwa katika jeshi la Mungu. Tafuta cheo na nafasi yako katika ufalme wa Mungu na simama imara.

Najua tunazungumzia na kuzaliwa mara ya pili na hii yaweza fahamika kama ni jambo lisilo faa, lakini kumbuka katika kitabu cha Ufunuo, kinazungumza kuhusu mwanamke aliye kua na utungu wa kuji fungua mtoo. Jambo kuu ambalo ninalotaka kuchangia, ni kwamba mara tu unapozaliwa mara ya pili, Joka mwekundu (Shetani) yuko hapo ili akumeze. Hiyo yatuweka sisi sote tuliozaliwa mara ya pili katika vita ya kiroho. Kuna utungu wa kumzaa Kristo katika maisha yetu. Nimetumai na kuomba ya kwamba ujumbe huu mfupi utakuwezesha kukua katika neema na ufahamu wa Bwana wetu Yesu Kristo, na kujichunguza na kuona kama uko katika imani. Mungu awabariki.

Ndugu Rob Coones

Ujumbe huu na mafundisho mengine katika kanda ya Ndugu Mchungaji Rob Coones, yanapatikana katika mtandao, na umechapishwa na kugawanywa bila malipo. Kwa nakala au lugha nyingine zaidi, Andika kwa lugha ya Kingereza kwa anwani iliyo hapo chini, na eleza kiasa unayo hitaji kwa matumizi ya kazi ya Mungu.

Christian Temple Ministerial Association
3844 Mount Gilead Church Road
Sophia, NC 27350-8820 USA